Mahakama
ya Afrika ya haki za binadamu yenye makao yake makuu jijini Arusha
imetoa miezi sita kwa serikali ya Tanzania kuanza kutekeleza mchakato wa
kuwepo kwa mgombea binafsi katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.
Jaji mkuu wa mahakama hiyo Mh. Sophia Akufo amesema
kwa mujibu wa mkataba ulioridhiwa na nchi zote baada ya kutolewa kwa
hukumu ni lazima utekelezaji wake ufanyike ndani ya muda uliopangwa
utaratibu ambao bado haujafanyika baada ya hukumu ya kesi ya mgombea
binafi kutolewa mwezi June mwaka 2013 .
Aidha Mh Akufo
amefafanua kuwa pia serikali inawajibika kuweka hukumu maelekezo ya
hukumu iliyotolewa ya haki ya kuwepo kwa mgombea binafi katika gazeti la
serikali katika kipindi kisichozidi miezi tisa baada ya kutolewa
utaratibu ambao pia bado haujatekelezwa
Tarehe 14 June mwaka
2013 mahakama hiyo ilitoa hukumu ya kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi
iliyokuwa imewasilishwa mahakamani hapo na MTIKILA
No comments:
Post a Comment