Pages

Thursday, June 5, 2014

MTOTO WA MIAKA 7 AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO


MTOTO aliyefahamika kwa jina la Najma Benjamin (7) amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari maeneo ya Bayuni Sheratoni, Kata ya Chanika, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Ally Omary Mnzava, amesema kuwa huko Barabara ya Chanika, gari aina ya Toyota Noah yenye namba T 611 CUN ikiendeshwa na Kasimu Ally (22) mkazi wa Chanika Mwisho, imemgonga mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto huyo.
Mnzava amesema mtoto huyo amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari, ambapo dereva kwa sasa amekamatwa na maiti kuhifadhiwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili huku upelelezi ukiendelea.

No comments:

Post a Comment