Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha
kuwataarifu abiria wote na wananchi kwa
jumla kuwa kutokana na kukamilika
ukarabati wa daraja eneo la bonde la mto Ruvu mkoani Pwani huduma ya treni ya
abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne Juni 24, 2014 kutoka Stesheni ya Dar
es Salaam saa 11 jioni. Wananchi wanotaka kusafiri wafike stesheni zilizo karibu
yao kwa ajili ya kukata tiketi kuanzia Juni 19, 2014.Halikadhalika muda wa
kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya Dar kwenda
Kigoma na Mwanza utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka Kigoma na Mwanza kuja
Dar katika siku za Alhamis na
Jumapili ni saa 11 jioni
kutokea Kigoma na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.
Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake. Uongozi wa TRL
unawapongeza wananchi kwa ujumula kwa ushirikiano na uvumilivu waliouonesha
wakati wakisubiri kukamilika kwa kazi ukarabati wa njia ya reli.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano ya
TRL kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Juni 18, 2014.
No comments:
Post a Comment