‘’MATESO
basi, damu ya Yesu yatosha’’. Hiyo ni kaulimbiu iliyotolewa katika
Kanisa la Nchi ya Ahadi lililopo Sinza-Kamanyola jijini Dar, chini ya
Mchungaji Kiongozi Harris Kapiga, wakati wa maombi maalumu kwa ajili ya
wasanii wa Bongo Muvi ili kuvunja roho ya mauti juu ya tasnia hiyo ya
filamu ambayo imewakumba wasanii wake.
Maombi hayo pia yalikuwa ni kuwaombea ulinzi wote waliomo na wanaotamani kuingia katika tasnia hiyo.
Maombi
hayo yaliwakilishwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),
Saimon Mwakifwamba, wasanii na waimbaji Bahati Bukuku, Dotnata na
wengineo.
No comments:
Post a Comment