Polisi nchini Malawi wamefyatua gesi ya kutoa machozi
kuwasambaratisha waandamanaji wanaodai kuhesabiwa tena kura za uchaguzi wa rais
zilizopigwa wiki iliyopita.Waandamanaji walichoma matairi na waliharibu maduka
Ijumaa katika mji mkuu Lilongwe kabla ya kilichotarajiwa na mahakama kuu nchini
humo kutangazwa kama matokeo ya uchaguzi uliokuwa na mzozo yatatolewa hadharani
au kura zitarudiwa kuhesabiwa.Uchaguzi uligubikwa na matatizo yakiwemo kuchelewa
kufunguliwa kwa vituo vya kupiga kura na kasoro nyingine kwenye karatasi za
uchaguzi. Matatizo hayo yalichochea tume ya uchaguzi nchini humo kuongeza muda
wa kupiga kura kwa siku moja zaidi na kisha siku ya tatu upigaji kura
ulifanyika kwenye baadhi ya maeneo.
Wakati huo huo Rais Joyce Banda anasema uchaguzi uligubikwa
na wizi mkubwa ikiwemo wizi wa kuongeza kura katika masanduku ya kupigia kura
na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.Aliagiza uchaguzi mpya ufanyike ndani ya
muda wa siku 90 na alisema hatokuwa mgombea katika duru hiyo ya upigaji kura.
Lakini mahakama kuu ilipuuzia matamshi yake wakati chama kikuu cha upinzani
kilipolalamika.CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment