Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 6, 2014

SHUHUDIA MZIGO ULIOSHUSHWA NA CHADEMA KATIKA KUMARISHA CHAMA


Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeingiza pikipiki 252 zitakazo tawanywa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha zoezi la CHADEMA ni msingi ambalo linaendelea nchi nzima likisimamiwa na kanda zilizoundwa mapema mwaka jana (2013), huu ni muendelezo wa kuziwezesha kanda ziweze kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi kwa maendeleo endelevu ya chama.

Pikipiki hizo pia zitakuwa msaada mkubwa katika kipindi hiki ambapo chaguzi ndani ya chama zinaendelea kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini, lakini pia ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji unao tarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.

Lakini pia itakuwa muendelezo wa kuziimarisha kanda za chama, kama mtakumbuka kwenye uzinduzi wa kanda kila kanda ilipatiwa gari mpya aina ya Ford Ranger, Pikipiki mpya zenye brand ya CHADEMA M4C zaidi 126 zenye PA system zenye uwezo wakuhutubia umati wa watu kuanzia 500 hadi 1000 na Megaphone ndogo zaidi ya 256



Sehemu ya Shehena ya pikipi zilizowaingizwa jana



Wakati watendaji wa chama makao makuu wakiwa busy na kushirik kupokea pikipiki hizo, jana kuna uzi uliwekwa hapa ukiwa na kichwa "Watendaji wa CHADEMA makao makuu kugoma", na eti wanataka kumfungia katibu mkuu Dr Slaa ofisini ili kushinikiza kuongeza mishahara; Tuliupuuza kwa kuwa haukuwa na ukweli wowote bali ulijaa hekaya za kutunga zisizo kuwa na msingi kwa kuwa CHADEMA kinafanya mambo yake kwa utaratibu.


Mapambano yanaendelea ili kuzidi kuwaamsha watanzania dhidi ya ufisadi, ubadhirifu wa mali na nyara za umma na ukandamizaji wa haki za binadamu. Mpaka kieleweke.

No comments:

Post a Comment