Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa inawezekana kwa wao kuwazalisha watoto kutoka kwa wazazi watatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Wanasayansi hao wanasema kuwa wanasubiri mabadiliko katika
sheria na badiliko katika mtazamo ya watu kabla hawajapandikiza manii kwa mayai
kutoka kwa wanawake wawili .Madaktari hao wa uzazi wanasema kuwa wanaweza
kuzalisha watoto wenye siha nzuri iwapo wataruhusiwa kisheria kuondoa magonjwa
kutoka kwenye chembechembe za uzazi na kupandikiza mbegu za kiume kutoka kwa
baba mzazi.Hata hivyo mipango hiyo tayari imevutia tahadhari kutoka kwa
halmashauri inayosimamia utabibu wa uzazi nchini Uingereza.
Inawezekana kuzalisha mtoto wazazi watatu
Huku ikibainika kuwa kunahaja ya mbegu za uzazi kusafishwa
na zile zenye maradhi kuchujwa kitaalamu bila ya kupoteza uwezo wa mama kumzaa
mtoto asiye na maradhi ya kurithi.Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kati ya
watoto 6500 wanaozaliwa kuna mmoja aliyeambukizwa maradhi kutoka kwa wazazi
wake kupitia celi zijulikanazo kama (mitochondria.) ambazo zinasababisha
maradhi kama kukosa nguvu mwilini kupofuka maradhi ya moyo na hata wengine
hufa.Watafiti na madaktari wa maswala ya uzazi chini ya nembo ya Human
Fertilisation and Embryology Authority (HFEA)waliohudhuria kongamano hilo
walishuhudia hatua kwa hatua jinsi utaalamu huu unaweza kumsaidia mama ambaye
anaseli za mwili zilizoambukizwa akisaidiwa kumzaa mtoto bila ya maradhi hayo
kwa usaidizi wa mwanamke mwenye seli nadhifu na yenye afya.
Prof Andy Greenfield alisema hawana hakika iwapo utalamu huu ni salama kutumika kwa binadamu hadi pale mtoto atazaliwa baada ya kutimika kwa teknolojia hii mpya.
Serikali kwa upande wake imeipungia teknolojia hii kwani itaisaidia jamii kutoathirika na magonjwa ambayo hurithishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Daktari mkuu , Prof Dame Sally Davies, akisema ni jambo la dharura ambalo serikali inasubiri tu kuafiki utafiti huo na kisha kupitisha sheria zitakazoruhusu watoto wenye wazazi watatu.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment