Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa
waliowasha vipaza sauti kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma ambapo
sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata hapa chini.
‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11
lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini
unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara kama
chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza ushuru kwenye
pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa na kuvuta inapungua
tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni kukusanya mapato, hiki ni kitu cha
kusikitisha sana’
‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama
chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida
Same serikali imeweka vikao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO
MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao
vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’
‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali
ingeweza kabisakabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme
mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingiza kwenye gridi ya taifa na mngeweza
kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’
‘Hata kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na
serikali ambayo haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado
inakopesheka, bado tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda
kukopa barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe,
ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali yenu
ihamie hapa Dodoma’
‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma,
ukiondoa serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo
hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu wakuu wote wa nchi watakuwa
wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua ni
Iringa, Mbeya na Singida hapa’
‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua
Mawaziri wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae
kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili hii
nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za Urais huko
kote anakokwenda’
No comments:
Post a Comment