Wanazingirwa: Nyota wa England, Daniel Sturridge na Chris Smalling wakizungukwa na mashabiiki walipokuwa bichi jana mjini Rio.
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya England kama kawaida yao hawakutaka kupoteza muda baada ya kuwasili Brazil ambapo walienda kupunga upepo bichi mjini Rio, huku Daniel Sturridge akiwa kivutio kikubwa kwa mashabiki.
Vijana wa Roy Hodgson wamefikia katika hoteli ya Royal Tulip ambapo wameweka kambi kwa ajili ya kombe la dunia na baada ya kufika, jana asubuhi walitumia muda kula bata kwa kuogolea baada ya safari ya saa 8 na nusu wakiwa angani kutokea Miami.
Lakini Sturridge, na wachezaji wenzake, Chris Smalling, Danny Welbeck na Jordan Henderson, waliamua kutoka kidogo eneo la hoteli na kwenda bichi.
Kipenzi cha mashabiki: Sturridge akisalimiana na shabiki kijana nje ya hoteli ya England
Mwandishi wa habari akijaribu kupata hata neno moja kutoka kwa mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck
Wachezaji wa England walizingirwa na waandishi wa habari za magazeti na TV, huku nao watoto wakifurahia kukutana na mashujaa wao.
Baadaye wachezaji walirudi hotelini baada ya kupata kijua na kukutana na mashabiki wao wa Brazil.
Welbeck akiwa amezingirwa na vijana wadogo, huku Smalling (kushoto) akifurahia kinywaji baridi
Wanarudi: Smalling (kushoto), Welbeck (katikati) na Jordan Henderson (kulia) wakirudi hotelini kwao.
No comments:
Post a Comment