Raia waliopiga kura nchini Afghanistan wakatwa vidole
Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki
akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kazkazini mwa taifa hilo
kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi
wa urais wa raundi ya pili.
Katika tukio jengine kundi la Taleban liliwakata vidole
baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.
Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu
ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Raia wa taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa waziri wa
maswala ya kigeni Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuhudumu kama
waziri wa fedha.
Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya
magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.
No comments:
Post a Comment