Mpiganaji: Rais wa Simba sc, Ismail Aden Rage ataendelea
kuiongoza klabu hiyo.
Wengi walijiuliza kwanini TFF imefikia uamuzi huo, lakini
Malinzi alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia
kuibuka kwa malalamiko
mengi ya kimaadili, hivyo kamati hiyo itayasikiliza na kufikia maamuzi.
Uchaguzi wa Simba uliopangwa kufanyika juni 29 mwaka huu
uliingia sura mpya tangu Michael Richard Wambura aliopoenguliwa kugombea nafasi
ya Urais.
Suala hilo lilionekana kugusa watu wengi, lakini alipokata
rufani na kushinda, mengi yakaibuka zaidi na baadhi ya wanachama walipinga
kurudishwa kwake katika uchaguzi wa Simba.
Hata hivyo, Malinzi amekiri kuwa TFF imepokea malalamiko
mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu
hiyo, hivyo ni muhimu kuundwa kwa kamati ya maadili itakayoshughulikia mambo
hayo.
Wakati huu ambapo kamati itakuwa ikiundwa, kamati ya
utendaji ya Simba iliyopo madarakani kwasasa, chini ya Rais wake, Ismail Aden
Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi
utakapokamilika.
Jana Rage wakati anazungumza na mtandao huu alisema
anajitahidi kuhakikisha anaacha mchoro au msingi au hata ghorofa moja ya
Hosteti za wachezaji katika eneo lake la Bunju ili kuepukana na gharama kubwa
wanazotumia kuwaweka wachezaji hotelini wanapofanya kambi.
Rage aliyasema hayo kufuatia uongozi wake kuanza utekelezaji
wa ujenzi wa uwanja wa kisasa ambapo tayari magereda na malori yalishapelekwa
kwajili ya kazi.
No comments:
Post a Comment