Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kugawa
Vitambulisho vya Taifa kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano na
Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, ilieleza kuwa huduma hiyo
ilianza kutolewa juzi ikianzia katika wilaya ya Temeke.
Kata ambazo NIDA imeanza kugawa Vitambulisho ni Mtoni,
Azimio, Tandika, Buza na Yombo Vituka ambapo katika kata hizi zoezi la ugawaji
litafanyika Juni 18 hadi 22, 2014.
Ilieleza kuwa majina ya waombaji wa vitambulisho
yamebandikwa kwenye mbao za matangazo za ofisi za Serikali ya Mitaa husika na
kwamba waombaji wanatakiwa kwenda na
risiti walizopewa na NIDA baada ya kuchukuliwa alama za vidole, kupigwa picha
na kuweka saini ya kielektroniki.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, huduma inatolewa kuanzia saa
2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni na kuwa Mamlaka inatumia njia mbalimbali za
mawasiliano kuwafikia walengwa katika zoezi hili.
SOURCE: NIPASHE
No comments:
Post a Comment