Pages

Thursday, June 19, 2014

WAMILIKI WA MTANDAO WA FACEBOOK WATOA MAELEZO JUU YA TATIZO LILITOKEA DUNIA NZIMA KWA FACEBOOK KUTOKUWA HEWANI KWA DK 30



Wamiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambao una watumiaji wengi zaidi duniani wamelazimika kutoa maelezo juu ya kuondoka hewani kwa mtandao huo kwa muda wa dakika 30 dunia nzima.



Msemaji wa Facebook amenukuliwa akisema kuwa “Mapema leo asubuhi tulipata tatizo kubwa la watu kushindwa kuingia na kuandika chochote au kupost picha katika mtandao wetu kwa muda wa dakika 30″
Anaendelea kwa kusema kuwa wametatua tatizo hilo haraka na kufanikiwa kurejesha mtandao huo hewani kwa asilimia 100 ambapo pia ameomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.



Wakati mtandao huo ukiwa chini na watu kushindwa kupost wengi walihamishia hasira zao kwa kuandika kupitia Twitter.

 
Asilimia 78 ya watu wanaotumia mtandao wa Facebook dunia nzima walishindwa kabisa kutumia mtandao huo kwa dakika 30 wakati asilimia 21 ya watu waliweza kuingia.

No comments:

Post a Comment