Watalii ndani ya Hifadhi ya Ruaha
makundi ya tembo wa Ruaha
makundi ya Simba wa hifadhi ya Ruha
IDADI ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa imeanza
kuongezeka ikiwa ni matokeo ya juhudi za uwekezaji na matangazo yanayofanywa na
wadau mbalimbali katika kuitangaza hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopota Afisa Utalii
Mwandamizi wa hifadhi hiyo, Eva Pwele alisema kumekuwepo na wastani wa ongezeko
la asilimia mbili ya watalii wa nje huku idadi ya wale wa ndani ikiwa ni ya
kuridhisha.
Akizungumza Na timu ya
wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo
hivikaribuni, Pwele alisema: “juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali na
TANAPA katika kuboresha miundombinu ya barabara za ndani na nje ya hifadhi
zimnatarajia kuongeza watalii wanaotembelea hifadhi hii.
Alisema pamoja na juhudi hizo Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) inaendelea na mchakato wa kupata wawekezaji watakaongeza huduma za
hoteli na uongozaji wa watalii ndani ya hifadhi.
Alisema wakati katika kipindi cha 2009/2010 watalii wa nje
waliotembelea hifadhi hiyo walikuwa 11,040 wale wa ndani ambao wanasaidia sana
kuamsha hali ya watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii walikuwa
8,039.
Kuanzia mwaka huo idadi yao iliongezeka na katika takwimu za
2010/2011, Pwele alisem wa nje walikuwa 12,885 na wa ndani 9,868 huku mwaka
2011/2012 wa nje wakiongezeka hadi 13,940 na wa ndani wakiwa 9,721.
Mhifadhi huyo alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013
watalii kutoka nje waliongezeka hadi 14,299 na wa ndani walifika 9,994.
“Ni matarajio yetu idadi ya watalii itaongezeka katika
kipindi hiki cha 2013/2014; hiyo yote ni kutokana na mambo mengi yanayofanywa
katika kuitangaza hifadhi hii yenye upekee,” alisema.
Alisema hifadhi ya Taifa ya Ruaha ipo katika eneo
linalokutanisha ukanda wa kaskazini mashariki na kusini mashariki mwa Afrika na
hivyo kuifanya iwe na aina mbalimbali za mimea na wanyama ambao baadhi yake hawapo katika hifadhi
nyingine.
Aliwataja naadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi
hiyo kuwa ni pamoja na idadi kubwa ya tembo kuliko hifadhi nyingine yoyote
Afrika Mshariki, aina 571 ya ndege wakiwemo wale wanaozunguka nchi mbalimbali,
swala, tandala mdogo na mkubwa, samba, nyati, pundamilia, twiga, boko,
mamba, chui, mbwamwitu, nyani, mbwea na
wengineo wengi.
Alisema katika hifadhi hiyo, wanafanya utali wa usiku ambao
husaidia watalii kuona wanyama wasioonekana mchana, utalii wa kutembea kwa
miguu ili kumfanya mtalii awe jirani na mazingira ya hifadhi na utalii wa
masafa marefu kwa kutumia magari.
Ili kufika katika hifadhi hiyo, watalii wanaweza kutumia
njia ya barabara kutoka mikoa mbalimbali kupitia Iringa Mjini au ndege kutoka
viwanja vya Arusha, Songwe Mbeya, Dodoma, Dar es Salaam na Nduli Iringa
No comments:
Post a Comment