Picha za kusikitisha za watu waliouawa na kujeruhiwa katika
shambulizi lililofanywa Mpeketono Jumapili usiku
Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu
na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.Shambulizi la leo
limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi
yaliyowaua watu 50 Jumatatu.Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia
kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na
kuambia shirika la habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi
itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika
usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha
polisi pamoja na kuteketeza magari.
BBC
No comments:
Post a Comment