Pages

Sunday, June 15, 2014

WATU 1O WAFARIKI MKOANI MBEYA


WATU 10 wamekufa katika matukio tofauti mkoani Mbeya likiwemo la mtoto mdogo, Joshua Shukrani (3), kugongwa na gari na mwanafunzi wa shule ya msingi Iduda, leus John (07), kufa kwa kugongwa na gari alipokuwa akivuka barabara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi, kwa vyombo vya habari Juni 9-13, 2014 ( tunayo nakala) imesema matukio hayo yametokea katika kipindi hicho na kuwataja waliokufa kuwa ni pamoja na, William kabinji (38) mkazi wa kijiji cha mantengu ‘A’ alikutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga sehemu za usoni na kisha kunyongwa na kutundikwa juu ya mti, Juni 08, 2014 katika kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbozi.
 
 Amesmea inadaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuchoma moto nyumba tatu za jirani zake na kuiteketeza nyumba ya, Elias mwamlima (32), Juni 04, 2014 na kutoroka na Ezekiel Kyando (72) mkazi wa Bagamoyo katika Wilaya ya Tukuyu aliyekufa kwa kugongwa na gari na dereva asiyefahamika mkazi Juni 8, 2014 saa 10:00 asubuhi.
 Kamanga Msangi aliendelea kwa kuwataja wengine  kuwa ni, Petro Kibona (30), aliyekufa kwa kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi mawe, fimbo na rungu tukio lililotokea Juni 10, 2014 saa 3:00 asubuhi kwa tuhuma za wizi wa pikipiki namba T.994 ARB aina ya Toyo, mali ya, Aron Baned (36) ambayo hadi sasa inashikiliwa kwa uchunguzi.
 "Juni 10, 2014, Wolter Jonathan (36) mkazi wa morogoro amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari na dereva asiyefahamika katika barabara Kuu ya Mbeya/Njombe katika kijiji cha Mbuyuni, Wilaya ya Mbarali mkoa wa mbeya ambapo chanzo cha ajali kinachunguzwa, alikimbia na gari mara baada ya tukio, na mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Iduda Leus John (7) alikufa papo hapo Juni 10, 2014 baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Coaster lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika na kukimbia baada ya tukio” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.Hata hivyo, Mwanaume asiyefahamika jina wala makazi (30-35) aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi waliojichukulia sheria mikononi wakitumia silaha za jadi fimbo, mawe na rungu kutokana na tukio la unyang’anyi wa pikipiki tukio lililotokea Juni 11, 2014 saa 11: oo jioni katika kijiji cha Idiga Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.

Uchunguzi wa kipolisi umeonyesha kuwa marehemu alimkodi mwendesha pikipiki yenye namba T773 CDJ aina ya T-better, Imani Emanuel (19), na walipofika mbele zaidi ndipo alijitokeza mtu mwingine na kwa pamoja walinyang’anya pikipiki na kisha kumfungwa mikono na miguu kwa mipira na kutoweka na pikipiki hiyo ambapo katika tukio jingine, Madawa Jaston (29), aliuawa kwa kuchomwa kisu kichwani, usoni na miguuni na mumewe, Joseph John (49) wote wakazi wa kijiji cha Isangati.
 Katika tukio lingine, Rashid Mfinanga (37) ‘dereva’ na Godeni Katemu (60), wamekufa baada ya gari lenye namba T.254 BFZ aina ya Mitsubishi fuso lililokuwa likiendeshwa na dereva Rashid Mfinanga, kupinduka na kuwaua papo hapo katika Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, na Mtoto mwenye umri wa miaka (3) Joshua Shukrani mkazi wa Ilemi kufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika namba za usajili mara moja.
 Taarifa za msako
Watu wawili, Braun kamwela (30), na Gabriel Mwambene (30), wote wakazi wa Kiwira wakiwa na TV aina ya Panasonic moja na Redio aina ya Sony mbili mali inayodhaniwa kuwa ya wizi.
 watuhumiwa walikamatwa juni 09, 2014 saa 9:00 usiku katika eneo la kiwira, Kata ya Kiwira, wilayani Rungwe na taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinafanywa na Samson Julius (18), akiwa na bangi kete 68 sawa na uzito wa gramu 340 mkazi wa kijiji cha NondeJuni 8.06.2014 saa 11:00 asubuhi katika eneo la stendi kuu ya mabasi, kata na tarafa ya Sisimba.
 “Juni 10, 2014 tulimshikilia Asajile Mwakisambwe (41) mkazi wa kijiji cha majengo kwa kosa la kukutwa na pombe haramu ya gongo yenye ujazo wa lita 52, na mfanyabiashara Jailos Jayange (45) mkazi wa Mbozi ameshikiliwa na Jeshi hilo Juni 12, 2014 akiwa na vipodozi mbalimbali vilivyopigwa marufuku na serikali katika Wilaya ya Momba.
 Wakutwa na note bandia
Watu watatu, Tatu Mwampashi (25), Angomwile Kapungu (26), wakazi wa mtaa wa Mnyamwanga wanashikiliwa wakiwa na noti bandia 62 kila moja ikiwa na thamani ya Tshs 5,000 sawa na Tshs 310,000 zote zikiwa na namba AA0845926 Juni 12, 2014, na mtuhumiwa mwingine Angomwile Kapungu (26) alikamatwa katika Kitongoji cha Sikanyika, Kata na Tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, akiwa na dola bandia 2 kila moja ikiwa na thamani ya USD 100 zikiwa na namba BL-72830434-a na FT-85311229-h na taratibu za kuwafikisha Mahakamani FiktaPevu imejulishwa kuwa zinaendelea.
 Wapiga debe tisa mbaroni
Jeshi hilo, linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kufanya fujo maeneo ya Stendi ya Mabasi Ilomba jiji humo kufuati mgomo wa daladala Juni 10, 2014.Watuhumiwa hao ni pamoja na, Ipyana Mwangomole (27), Hussein Hassan (32), Zakaria lianda (23), Bahati Mathias (28), Boniface Jasson (22), Amos Robert (16), Otto Jeki (21),  Alex mwaikuji (28), na Leofasi Anthony (17), wote wakazi wa jijini humo ambao wanatuhumiwa kwa kosa la kufanya fujo kufuatia mgomo wa daladala na taratibu za kufikishwa Mahakamani zinaendelea.

No comments:

Post a Comment