Yaya Toure, akiwa mazoezini jumatatu, anaendelea
kuimarika kwa kasi kuelekea mchezo wa ufunguzi.
KIUNGO wa Ivory Coast,Yaya Toure anaendelea kuimarika kwa
kasi kuelekea katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya Japan
jumamosi, amesema
kocha Sabri Lamouchi.
Toure ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake tangu
alipofanyiwa upasuaji mwezi uliopita.
Lamouchi amesema timu ya madaktari wa Ivory Coast inajitahidi sana kuhakikisha
mchezaji huyo bora wa mwaka wa Afrika anacheza wakati nchi yake itakapoanza
mchezo wa ufungizi wa kundi C dhidi ya Japan mjini Recife.
'Tunafanya kila linalowezekana ili acheze" kocha
aliwaambia waandishi wa habari.
Toure alipata majeruhi katikati ya mwezi aprili mwaka huu,
lakini alirudi uwanjani kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa wa pili katika
misimu mitatu.
Halafu akaenda Qatar kwa ajili ya matibabu na baadaye
alijiunga na kikosi cha Ivory Coast kwenye kambi ya mazoezi huko America.
Toure hakucheza mechi mbili za kupasha pasha dhidi ya Bosnia
na El Salvador
No comments:
Post a Comment