WAKATI Rais Dkt. Jakaya Kikwete anataraji kuwa mgeni rasmi wa kilele cha siku ya maadhimisho ya mazingira duniani yanayoadhimishwa kitaifa Juni 5 mwaka huu mkoani Mwanza, uchafuzi wa mazingira mto Mirogo umeongezeka jijini hapa.Imebainika kuwa, Kaya 75 jijini humo zinatirilisha vinyesi na majitaka ndani ya Mto Mirongo unaomwaga maji machafu Ziwa Victoria hali ambayo imedaiwa kuongezaka kwa kasi ya uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa mto huo hivyo kuhatarisha afya watumiaji wa maji ikiwemo wanyama, mimea na viumbe hai waishio majini.
Hali hiyo pia ilijitokeza na kushuhudiwa na baadhi ya wadau
wa mazingira kutoka Menejimenti ya Ofisi za Maji Bonde la Ziwa Victoria,
Maafisa Afya wa Jiji la Mwanza na Jumuia ya waumiaji wa maji na mazingira
walipokuwa wakifanya zoezi la kufafisha mto Mirongo hii leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la daraja la
Mabatini linalopitiwa na mto huo baada ya kubaini kuwepo kwa Kaya hizo, Kaimu
Afisa wa Maji kutoka Bonde la Ziwa Victoria Godfrey Kajanja alisema kwamba,
Ofisi yake na Halmashauri ya Jiji zitakutana kuchukua hatua za kisheria kwa
Kaya hizo na watu walio na tabia ya kuchafua maji ya mito.
Kajanja alisema kwamba, hali hiyo ikiachwa kuendelea bila
kudhibitiwa kutawezesha kuibuka magonjwa ya tumbo endapo Mamlaka ya Majisafi na
Mazingira ya jijini humo haitachukua hatua za kuongeza kiasi kikubwa cha dawa
ya kutibu maji kabla ya kusambazwa kwa watumiaji.
“Lazima sasa tushirikiane kuzitekeleza sheria zilizopo za
Mipango miji kwa upande wa Jiji la Mwanza, pamoja na ofisi yetu ya Bonde
kutumia sheria ya usimamizi wa rasilimali ya maji Na. 11/2009 na sheria ya
usimamizi wa mazingira Na. 24/2004 ambazo zinaoanisha adhabu ya fedha na
kifungo kwa watu watakaokaidi na kukutwa na makosa,” alisema.Kwa upande wake
Mhandisi wa Maji toka ofisi za Bonde la Ziwa Victoria Mhandisi Jane John
alieleza kwamba, hatua hivyo inatakiwa kukomeshwa mara moja na jamii iliyo
kandokando ya maeneo unapipita mto Miringo na maeneo ya vyanzo vya maji ili
kusaidia kulinda na tabia ya uchafuzi wa mazingira ikiwemo udhibiti jambo ambalo
litaepusha uharibifu na uchafuzi.
“Tumeshuhudia mabomba ya vinyesi na maji machafu yakimwaga mtoni
wakati tukifanya usafi wa pamoja kwenye mto Mirongo na wadau mbalimbali walioko
kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira kitaifa hili ni jambo ambalo linahitaji
hatua za haraka kulikomesha na kuwachukulia hatua wanaofanya uchafuzi
huu,”alisisitiza.Naye Mwenyekiti wa NGO ya Jumuiya ya watumiaji maji na
mazingira Adam Shija ya Kata ya Mbugani Wilayani Nyamagana mkoani hapa alisema
kwamba, tumekuwa na changamoto kubwa wakati wa usafishaji wa mto huo na
wamebaini kuwepo kwa baadhi ya Kaya 75 ambazo zimekuwa zikitirilisha uchafu wa
vinyesi na majimachafu ndani ya mabomba yaliyoelekezwa mtoni humo.
Shija alifafanua walipotembelea kandokando yam to huo kwenye
maeneo ya unapoanzia na kupitia kasha kumwaga maji ziwani Victoria katika Kata
za Nyakato walibaini kaya 16, Mahina kaya 8, Mbugani kaya 24, Mirongo kaya 17,
Nyamagana kaya 6 na Pamba kaya 4 na tayari orodha hiyo imetokana na ukaguzi wa
Jumuiya hiyo hivi karibuni.
Wito wangu kwa Serikali na Idara zenye jukumla la kusimamia
rasilimali ya maji na mito, mabwawa na ziwa Victoria kutekeleza sheria kwa
vitendo ili kukomesha tabia hiyo ya uchafuzi wa maji na uharibifu wa mazingira
unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya wananchi bila kujali kama husababisha
madhala kwa watumiaji wa maji na kuhatarisha uhai wa viumbe hai majini.CHANZO GSENGO
No comments:
Post a Comment