Stori: Joseph Shaluwa
AFYA ya mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik
ambaye anatumikia Radio One Sterio ya jijini Dar es Salaam, si nzuri kiasi cha
kulazimika kufanyiwa upasuaji haraka.
Mtangazaji wa Radio
One Sterio mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik akifanyiwa upasuaji.
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa,
Abou alizidiwa ghafla Jumamosi ya Julai 26, mwaka huu akiwa kazini kwake na
kukimbizwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
“Alikuwa mzima kabisa, alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hindu
Mandal ambapo alifanyiwa upasuaji,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua aina ya upasuaji
aliofanyiwa Abou, chanzo kikafunguka: “Ndugu yangu, suala la ugonjwa ni siri ya
mgonjwa na daktari wake, labda uwasiliane naye, maana ametoka hospitali leo
asubuhi (Jumatatu), ana nafuu nzuri.”
Aboubakar Sadik akiwa Hospitali ya Hindu Mandal, Posta
jijini Dar es Salaam.
Baadaye mchana chanzo hicho kilimtumia picha mbalimbali za
Abou akiwa hospitalini hapo, ikiwemo aliyokuwa chumba cha upasuaji wakati
shughuli ikiendelea.
Mwandishi wetu alipomtafuta mtangazaji huyo kupitia simu
yake ya mkononi, hakupokea hivyo akalazimika kumtumia ujumbe uliosomeka: “Pole
kaka, nimepata taarifa unaumwa. Nini zaidi? Unaendeleaje sasa?”
Muda mfupi kabla ya kuelekea mitamboni, Abou alijibu:
“Shukrani kaka. Ni kweli, nilifanyia surgery (upasuaji) Hindu Mandal, lakini
nimesharuhusiwa, nashukuru Mungu ilikwenda vizuri.”
Abou anawika na vipindi mbalimbali Radio One vikiwemo Nani
Zaidi, Chombeza Time, Mtaa wa Mangoma na Flavor 120.Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment