Je unamkumbuka mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson ambaye
alikata Uume wake mwezi Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja
mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu
alipokuwa anafanya hivyo.
Johnson, aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya,
kufuatia kitendo chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi
Aprili. Madaktari walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya
mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.Lakini
aliamua wiki hii kujieleza kwa nini
alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha
televisheni cha E! nchini Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya ,
lakini nilikuwa najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu
hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu. Suluhu langu kwa masaiibu yangu ni
kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu,
'mini ni mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi.
Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''
Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa
na matatizo ya kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio
kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini
daktari alimwambia hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo
sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo
nafurahi niko hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu.
No comments:
Post a Comment