Hausigeli aliyedaiwa kuteswa na mtuhumiwa huyoMwanamke
Yasinta Rwechengura, mkazi wa Boko wilayani Kinondoni, Dar anayekabiliwa na
kesi ya kutuhumiwa kumtesa hausigeli wake kwa miaka miwili (siku 730),
amejikuta akihenyeshwa mahakamani.Hayo yamemkuta juzi alipofikishwa kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Kinondoni kujibu tuhuma
zinazomkabili ambapo alikuwa akipokea amri kutoka kwa askari na kumfanya kukosa
raha.
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi.
Msala huo unagusa hisia za wengi ndiyo maana watu kutoka
viunga mbalimbali vya Jiji la Dar walifurika mahakamani hapo kusikiliza
mwenendo wa kesi hiyo iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi, Boniphace Lihamwike.
Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye
alikuwa upande wa jamhuri, Mohamed Salum alisema anaiomba
mahakama hiyo kutotoa dhamana kwa
mtuhumiwa kwa sababu za kiusalama.
Sababu ya pili alisema bado hali ya mgonjwa ni mbaya na
amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akipelekwa mahabusu.
Kesi hiyo ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu na wanaharakati wa
haki za binadamu, awali ilikuwa
inasikilizwa na Hakimu Suleiman Mzava ambaye juzi hakufika mahakamani hapo kutokana na uhamisho alioupata na badala
yake kesi hiyo ilitajwa kwa Hakimu
Lihamwike.
Upande unaomtetea mtuhumiwa huyo uliokuwa ukiongozwa na
wakili wa kujitegemea, Msomi Gidion, uliiomba mahakama kumpa mteja wao dhamana
lakini ukagonga mwamba.
Hata hivyo, wakili Mohamed aliendelea kuiomba mahakama kwa
mara nyingine kutotoa dhamana kwa
mtuhumiwa kwa sababu alizozitoa awali.
Wananchi wakimshangaa
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alisema pande zote
zilikuwa na hoja akianza na upande wa mtuhumiwa ambapo alitoa ufafanuzi kuwa ni
haki yake ya kikatiba kupata dhamana
lakini upande wa jamhuri nao ulikuwa na hoja.
Hakimu huyo alisema kuwa shauri hilo kwa mara ya kwanza lilianzia kwa hakimu mwingine
na ndani ya faili la kesi hiyo hakukuwa na vielelezo vyovyote hivyo kuirudisha
kesi hiyo kwa hakimu kiongozi kwa ajili ya kupangiwa hakimu atakayeisikiliza.
Baada ya hapo, mtuhumiwa alipandishwa kwenye karandinga na
kurudishwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar kuendelea kuhenya hadi
atakapopata dhamana huku wananchi waliofika mahakamani hapo wakimshangaa.
No comments:
Post a Comment