Pages

Tuesday, July 22, 2014

BALOZI MDOGO WA TANZANIA NCHINI DUBAI ALIPOTEMBELEA KAMPUNI KUBWA YA UJENZI WA NYUMBA KULIKO ZOTE DUBAI



Mhe. Omar Mjenga, leo amepata fursa ya kuitembelea kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai, kwa lengo la kujionea miradi mikubwa iliyotekelezwa na kampuni hiyo.

Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.


Kufuatia mazungumzo kati ya Mhe. Mjenga na Bw. Rashid Lootah, mwenyekiti wa NAKHEEL, wamekubaliana kwa pamoja kuwa mwenyekiti huyo na ujumbe wa washauri na wataalam wake kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania, tarehe 10 hadi 13 Agosti, 2014.

Wakiongozana na Mhe. Balozi Mdogo Mjenga, watakutana na taasisi mbali mbali zikiwamo NHC, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), TTB, TANAPA na zingine nyingi. Aidha, watapata fursa ya kuongea na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Viwanda na Biashara, Ardhi, 
Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Kampuni hiu ina nia ya kuwekeza katika hotel za nyota tano, nyumba za makazi na biashara pamoja na maduka makubwa(shopping malls).









No comments:

Post a Comment