Pages

Tuesday, July 1, 2014

Basi la Lushanga laua mmoja na kujeruhi wawili Sengerema


Kijana ambaye ni dereva wa toroli la miguu minne jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 amefariki dunia papo hapo na kupasuka Kichwa baada ya kugongwa na basi la abiria lililokuwa likitokea mkoa wa Geita kuelekea jijini Mwanza kwenye makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Kijana huyo pia alikuwa akiendesha Pikipiki bila kuvaa “Helmet” huenda ingemsaidia asipasuke Kichwa.(Picha na Zainul Mzige).

Na MOblog, Sengerema
Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina lake mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38
(mwanaume) kufa papo hapo Na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari kwenye makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Tukio hilo limetokea jana Juni 30 majira ya saa 9 alasiri ambapo basi la abiria mali ya kampuni ya Lushanga lenye namba za usajili T 312 ATA likiwa na Abiria likitokea Mkoa wa Geita kuleleka mkoani Mwanza kupitia kivuko cha Kamanga.
Marehemu alikuwa anaendesha troli lililokuwa limebeba miti ambapo amepasuka kichwa na kusababisha Ubongo kutoka nje, na mwili wake umepelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na majeruhi kwa ajili ya matibabu.


Baadhi ya wakazi wa Sengerema wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kijana mwingine aliyepasuka eneo la jichoni baada ya ajali hiyo kutokea. Kijana huyo alionekana kuchanganyikiwa pamoja na maumivu makali baada ya kutokea ajali hiyo.
Kwa upande wa mashuhuda abiria waliokuwa katika basi hilo hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na gari hilo kuharibika baada ya kushindwa kuendelea na safari hivyo kurudi nyuma na kujikita kwenye mtaro.
Hadi tunaandika habari hii chanzo cha ajali hii hakijajulikana kutokana na uchunguzi wa polisi wilayani humo kuhusu ajali hiyo kuendelea na dereva wa basi hilo na konda wake waliotokomea kusikojulikana kutokana na mkusanyiko wa watu eneo la tukio.
Tutakuletea taarifa zaidi baada ya Polisi kutoa ripoti ya chanzo cha ajali hiyo.


Raia wema wakijaribu kumtuliza mmoja wa majeruhi alale chini kwa muda kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kuasuka eneo la karibu na  jicho lake huku mwendesha Baiskeli naye akiwa amepoteza fahamu kwa muda.





No comments:

Post a Comment