Pages

Sunday, July 27, 2014

CHADEMA MAKETE WAFANYA UCHAGUZI MKUU KWA MARA YA KWANZA‏

 Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
Kwa mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya.
 

Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw. Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6 na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1

Bw. Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho, wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake

Mbali na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26

Aidha Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake na wote wamepita bila kupingwa

Bi. Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa

katika uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la wazee wilaya

Katika hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.

Akiahirisha mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama

"Makamanda uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe ushirikiano" amesema Ngogo
Na Edwin Moshi, Makete

No comments:

Post a Comment