Oscar Dao ni Fundi cherehani nchini Burkina Faso.
Anashughulika kushona kile kinachomalizika kuwa chupi ya mwanamke ya rangi ya
waridi.
"Ni furaha kubwa kutengeneza vitu vizuri kama hivi, vya
kiwango cha juu," anatania fundi huyo mwenye miaka 36.Akiendelea na
shughuli kwenye cherehani chake katika duka la Copromof katika mji mkuu
Ouagadougou, Fundi Dao anafanya mabadiliko taratibu.
Huku kukiwepo mzozo wa pamba magharibi mwa Afrika, na wakati
kampuni za mitindo Ulaya zimehamisha utengenazaji bidhaa Asia, Kampuni ya
kutengeneza chupi ya Ufaransa, Atelier Augusti imeamua kutengeneza nguo za
ndani za wanawake Ouagadougou.
Therese Tiema pia hushona nguo binafsi kama sare za shule
Mmiliki duka hilo, Therese Tiema, ameajiri wafanyakazi
watatu zaidi katika miaka miwili iliyopita - na kuiweka idadi ya mafundi
cherehani aliyowaajiri kuwa tisa kati ya vyerehani 15, wanaoshona chupi
zilizoagizwa na kampuni hiyo ya Ufaransa."bado tunashona nguo binafsi
lakini tunajaribu kuondoka kwenye soko hilo na kuishia kupokea maagizo
makubwa".
Kutoka Afrika hadi Ufaransa
Atelier Augusti ni kampuni inayomilikiwa na dada wawili
Julie na Claudie Ramirez walioizuru Burkina Faso kwa mara ya kwanza miaka
misita iliyopita baada ya mama yao kuolewa na raia wa huko.
"kwetu haikuwa uamuzi kati ya kutengeneza nguo hizi
katika eneo la mashriki au Afrika," anasma Claudie Ramirez mwenye umri wa
miaka 27.
"daima ilikuwa ni Afrika, licha ya kwamba ingekuwa
rahisi kuzitengeneza katika eneo hilo la mashriki," anasema.Ndugu hao
wanataka chupi hizo zitengenezwe kwa kutumia pamba asilia ambaoyo huinunua
kutoka kiwanda kikubwa cha nguo cha Comatexkatika nchi jirani ya Mali.
"Hatahivyo ni lazima tutume mipira na wino wa chaa ya
kampuni kutoka Ufaransa. Kiwango tunachokihitaji hakipatikaniBurkina
Faso."
Kila chupi hukatwa na kushonwa kivyake
Chupi hizo zinauzwa kwenye mtandao na pia
katika maduka
manne nchini Ufaransa likiwemo moja katika mji mkuu, Paris.Claudie anasema
kuuza chupi hizo Burkina Faso inakuwa vigumu kwa sababu bei yake ambayo ni dola
25, ipo juu zaidi ya bei ya chupi zengine zinazonunuliwa nchini humo.
Mmiliki wa duka la Copromof wanakoshona mafundi, Tiema
anakubaliana na hilo: "sokoni unaweza kununua kwa bei rahisi chupi za
kutoka China, lakini zina madhara kwenye ngozi."
"Nina hakika kungekuwa na soko kwa chupi
zilizotengenezwa vizuri kwa pamba asili zilizonuiliwa miili ya Waafrika".
No comments:
Post a Comment