Chelsea wamethibitisha kumsajili rasmi Diego Costa baada ya kufikia makubaliano na Atletico Madrid.
Chelsea ilitaka kukamilisha usajili huo kabla ya
Kombe la Dunia kwa pauni milioni 32. Jambo hilo halikufanikiwa lakini sasa mkataba umefikiwa. Taarifa iliyotolewa imesema: "Chelsea inathibitisha kufikia makubaliano na Atletico Madrid kwa ajili ya uhamisho wa Diego Costa".
Chelsea walikuwa wamekubali kulipa ada ya uhamisho na Diego Costa mwenyewe aliwaambia Atletico hamu yake ya kuondoka, lakini mkataba ulikuwa mgumu kufikiwa.
No comments:
Post a Comment