Watu watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kwasunga
wilayani Handeni wamekufa baada ya kula futari ya mihogo inayosadikiwa kuwa na
sumu.Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Tanga, Constantine Massawe alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku
eneo la Kwasunga Handeni na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Handeni.Kamanda Massawe aliwataja waliokufa kuwa
ni Juma Jumbe (6), Abdi Jumbe
(10) na Ramadhani Jumbe (15). Pia alisema kuwa wazazi wa watoto waliwahishwa
hospitali ambako walipatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.
Kamanda Massawe alisema kwa mujibu wa wazazi wa watoto hao,
walikula futari hiyo na baada ya kumaliza, walianza kujihisi vibaya sambamba na
kuishiwa nguvu na alianza kuanguka mmoja baada ya mwingine.“Chanzo cha kifo ni
futari ya mihogo ambayo kwa mujibu wa vipimo ilikuwa na sumu. Wazazi wao wako
hai ila nao walikuwa katika hali mbaya, lakini baada ya kupatiwa matibabu
wanaendelea vizuri,” alisema kamanda huyo.Kamanda huyo aliwataka wote walio
katika mfungo kuichunguza mihogo wanayoinunua kwa ajili ya matumizi ya futari
kwani baadhi haifai kuliwa na binadamu.Mhogo unajulikana vyema. Kama mtu
ukiumenya na kuona una rangi za ajabu ajabu ndani, basi achana nao usiupike
mingine haifai kuliwa na binadamu,” alisema Massawe. Alitoa wito kwa watu kuwa
makini. (MWANANCHI)
No comments:
Post a Comment