skip to main |
skip to sidebar
HIZI NDO Nyumba watakazojengewa Okwi, Niyonzima, na wachezaji wote wa Yanga Zitazame Hapa
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba
za Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake
kupitia program maalumu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika
jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa
NSSF, Crecentius Magori alisema wachezaji wanapaswa kuona fahari
kumiliki nyuma au ardhi mjini, si magari.
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao
walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi
huo uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es
Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za
kisasa zaidi, hivyo ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba,
mkitoa kiasi nanyi muwe wamiliki wa nyumba hizo. “Kama utamudu na kutoa
kiasi cha sh. mil.8 na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo, NSSF watawapa
ufunguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi kwa miaka 15, kisha
unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo,” alisema Magori. Aliongeza kuwa
hata ikitokea mchezaji akafariki dunia, nyumba hiyo itaendelea kuwa mali
ya familia ya mhusika kwani itakuwa imerithiwa huku akisihi wachezaji
ambao si wanachama wa NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu,
alisema makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa
klabu hiyo, Yusuf Manji na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau.
Alisema lengo ni kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa
kumiliki nyumba ikiwa ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na
manufaa yake wakati anacheza, hata baada ya kustaafu soka
KATIBU MKUU WA YANGA, BENO NJOVU, ALIKUWEPO.
MAXIMO, MSAIDIZI WAKE LEIVA, SALVATORY EDWARD WAKISIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA.
MPOGOLO NA JACOB, WALIKUWEPO.
BAADHI YA MIJENGO.
No comments:
Post a Comment