Wafanyakazi wa dharura wa Ukraine wanasema wamekuta miili ya
watu 196 katika eneo ilipotokea ajali ya ndege yaMalaysia ya MH17.Jumla ya watu
298 walikuwemo ndani ya ndege hiyo wakati iliporipotiwa kutunguliwa katika eneo
linaloshikiliwa na waasi la ukanda wa Donetsk siku ya Alhamis.Nchi za Magharibi
zimekosoa vikwazo vinavyowekwa katika eneo ilipotokea ajali na kuitaka serikali
ya Urusi kuweka shinikizo kwa serikali ya Ukraine kuruhusu kuingia katika eneo
hilo.
Waangalizi wa kimataifa wanatarajia kutembelea eneo hilo
tena hapo baadae.
Serikali zote Ukraine na Urusi zimetuhumiana kwa kuitungua
ndege hiyo iliyokuwa ikiruka kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur.
No comments:
Post a Comment