Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia
sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.sabuni hizo zinadaiwa
kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa kushiriki
tendo la ngono na mwanaume.
Baadhi ya wasichana waliohijiwa na
BBC mjini Nairobi
wamekiri kutumia sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na
kurejesha hali ya ubikira.
Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini
Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni
hatari.
Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali
kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani.
No comments:
Post a Comment