Je unajua kwamba samaki hasahau?
Mtu huambiwa ana akili ya kusahau kama samaki. Lakini sasa
huenda hilo likabadilika baada ya wanasayansi kugundua kwamba, kinyume na imani
hiyo, baadhi ya samaki wanaweza kuhifadhi taarifa kuhusu mazingira waliomo kwa
takriban wiki mbili.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha MacEwan, waliwazoezesha
baadhi ya samaki wa Kiafrika wajulikanao kama cichlids, kuingia katika eneo
maalum la tangisamaki ili kupata chakula.
Walitolewa na siku kumi na mbili baadaye walirudishwa tena
ndani ya tangi samaki hilo, na saamki hao walionekana kuipendelea sehemu hiyo
maalum waliokuwa wakipewa chakula.
Watafiti hao wanasema ongezeko hilo la muda wa samaki
kukumbuka, huenda likampa samaki nafasi ya kuishi zaidi hususan wakati kuna
upungufu wa chakula.
"Samaki wanaoweza kukumbuka mahali chakula kilipo, wana
uwezo wa kuishi zaidi kuliko wale ambao hawakumbuki," alisema mwandishi
mwenza wa ripoti ya utafiti huo Trevor Hamilton, ambaye ni mwanasayansi wa chuo
hicho kikuu cha MacEwan nchini Canada,
Alisema samaki wanaweza kukumbuka kwamba sehemu maalum ina
chakula bila kuwepo tishio la samaki wanaoweza kuwaua, na hivyo wataweza kurudi
tena katika sehemu ile.
Wanasayansi hao wanasema samaki wakiwa baharini, ni muhimu
waweze kutambua maeneo yalio na chakula ili waweze kuendelea kuishi.
No comments:
Post a Comment