Joe Hart akiokoa mpira uliopigwa na Philippe Coutinho wakati wa mechi ya kirafiki mjini New York
MAJOGOO wa jiji, Liverpool waliwalaza mabingwa wa England, Manchester City kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya Uwanja wa Yankee, nchini Marekani.
Mabao ya kikosi cha Brendan Rodgers yalifungwa na Jordan Henderson katika dakika ya 59 na kinda Raheem Sterling mnamo dakika ya 85.
Magoli ya Man City inayonolewa na kocha raia wa Chile, Manuel Pellegrini yalifungwa na Stevan Jovetic dakika za 53 na 67 .
Wakati wa upigaji wa Mikwaju ya penalti Yaya Toure na Jesus Navas walishindwa kuzamisha mpira nyavuni baada ya kuokolewa na Mignolet, wakati huo huo Aleksandar Kolarov naye alikosa - hivyo kumpa nafasi Lucas Leiva kuipa ushindi wa 3-1 timu ya Liverpool. Penati pekee ya Man City ilifungwa Iheanacho.
Sturridge pia alipaisha penalti yake, lakini Emre Can na Henderson walifunga kabla ya Lucas kutumbukiza penalti nyavuni.
Timu hiyo ya Merseysiders sasa itachuana na AC Milan mjini Charlotte Jumamosi ikiwa na nafasi ya kuongoza kundi lake- ili ikutane na mahasimu, Manchester United inayofundishwa na Louis van Gaal mjini Miami.
Mashabiki wa Liverpool walifurika uwanja wa Yankee mjini New York.
Kikosi cha Liverpool: Jones, Kelly (Johnson 46), Toure, Coates (Sakho 76), Enrique (Robinson 46), Gerrard (Lucas 76), Henderson, Allen (Can 65), Coutinho, Lambert (Sterling 46), Sturridge.
Wachezaji wa akiba : Mignolet, Ward, Suso, Ibe, Coady, Peterson.
Wafungaji wa magoli: Henderson 59, Sterling 85.
Kikosi cha Manchester City: Caballero (Hart 46), Clichy (Richards 70), Kolarov, Boyata, Nastasic, Fernando, Navas, Zuculini, Milner (Sinclair 46), Jovetic (Yaya Toure 70), Dzeko (Iheanacho 46).
Wachezaji wa akiba: Nasri, Negredo, Garcia, Rodwell, Rekik, Silva, Wright, Lawlor, Huws, Guidetti, Bossaerts, Denayer.
Mfunagiji wa mabao: Jovetic 53, 67.
Nyota wa Man City Edin Dzeko akijaribu kumtoka mchezaji wa Liverpool
CHANZO BARAKA MPEJA
No comments:
Post a Comment