Mtoto (kulia jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 anayemtuhumu baba yake kumfundisha uchawi.
MTOTO mmoja
mkazi wa Kimara Salanga, jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa)
mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni aliibuka na kutoa madai mazito,
akimtuhumu baba yake mkubwa kuwa alimfundisha uchawi, Ijumaa lina mkasa
kamili.
Akizungumza
na gazeti hili hivi karibuni, mtoto huyo alisema alianza kufundishwa
tabia hiyo mbaya na baba yake mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka
mitano jijini Mbeya, kwa kumwelekeza namna ya kuroga na kuua watu.
Katika
mojawapo ya matukio makubwa aliyodai kuwahi kuyafanya ni pamoja na
kutengeneza ajali ya boti iliyotokea Nungwi mapema mwaka huu ambapo yeye
na wenzake walitumwa na baba yake huyo kutega mambo yao huku wengine
wakipanda kwenye chombo hicho ili kuongeza uzito uliosababisha boti hiyo
kuzama na kuua watu kibao.
“Tuligandisha
maji na kuweka sindano ambazo zilitoboa na baada ya watu kufa
tulichukua nyama na damu kwa ajili ya kula na kunywa. Kwa hiyo nimeua na
kula nyama za watu.
Baadhi ya tunguli za uchawi zilizokuwa zikitumiwa na mtoto huyo.
“Pia
niliwahi kutumwa kwa msichana ambaye nilimnyunyizia dawa, nikamkalia na
kumkaba shingoni mpaka akafa, nikamchukua na kumpeleka kwa baba mkubwa,
pale kitandani niliacha gogo ambalo lina sura yake, kule tulimla na
kunywa damu yake sisi na wachawi wenzetu.
“Baada
ya kufanya matukio hayo mazito, baadhi ya wananchi waliponigundua kuwa
ni mchawi, walienda kunishtaki kwa mama yangu mzazi, wakimwambia
asiponihamisha wataniua.
“Kwa
hali hiyo, huyu mjomba wangu akanileta Dar kwa ajili ya kufanyiwa
maombi, lakini siku ya kwanza tu baada ya kufika, wakati nakwenda
kuchota maji nilikutana na mmoja (jina limehifadhiwa) aliyeniambia kumbe
mimi ni kijana wa kazi, alinitambua kutokana na nyota tunayobandikwa
kwenye paji la uso baada ya kujiunga na uchawi ambayo ukikutana na
mwenzako mnatambuana.“Baada ya kuniambia hivyo, usiku wake nikiwa
nimelala, baba mkubwa alikuja kichawi na kunichukuwa na kunipeleka kwa
yule mzee ambaye ndiye mkuu wa wachawi wa eneo hili, akanikabidhi kwake
na mikoba yangu ya kichawi na hapo ndipo nikaendelea na kazi kwa upande
wa huku Dar nikishirikiana na wachawi wengine.
“Kazi
yetu mara nyingi ni kuloga, kuua na kunyunyizia dawa kwenye makaburi,
yakifunguka tunachukuwa nyama za watu na mafuvu na kuyapeleka nyumbani
kwa yule mkuu wa wachawi wa eneo hili tunapokutania.
“Hapa
nyumbani kwa mjomba niliweka dawa kwenye ukingo wa nyumba ili
wasimalizie kujenga na kumloga mkewe ambaye tulimtupia vidonda vya
tumbo, nilitaka kumuua lakini maombi yalimsaidia,” anasimulia kijana
huyo.
ATINGISHA KIJIJI CHA SALANGA
Kwa
mujibu wa shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Lucy, baada ya
kufanyiwa maombi kanisani kwa Mwingira, mtoto huyo alikiri kuachana na
uchawi lakini alikuja kugundua bado anaendelea kutokana na kufanya
maombi ya kufunga ambapo aliona katika maono kuna dawa ameweka kwenye
nguo zake alizokuwa akipenda kuzivaa kila siku. Alipobanwa kwa vitisho
ndipo aliwataja wachawi wenzake na kuongeza kuwa kila alipokuwa akitoka
kwenye maombi, anakutana na wachawi wanamvisha uchawi tena na ule wa
tumboni aliolishwa bado unaendelea kufanya kazi.
WATINGA KWA MJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA
Baada
ya kueleza mambo hayo mazito waliamua kutinga kwa mjumbe ambaye baada
ya kuwasikiliza aliitisha kikao cha pamoja na yule mzee ambapo mtoto
huyo alieleza kinagaubaga mbele ya wananchi mambo wanayofanya wakiwa na
mzee huyo lakini alikataa na kuapa kwa kutumia msahafu kuwa anasingiziwa
na kwamba hajawahi kufanya mambo hayo.
NYUMBANI KWA MZEE ANAYEDAIWA MCHAWI
Mapaparazi
wetu walitinga nyumbani kwa mzee huyo ili azungumzie suala hilo lakini
jitihada ziligonga mwamba baada ya kumkosa ambapo mkewe anayedaiwa
kushirikiana naye kwenye mambo hayo, aliyejitambulisha kama mama Isha,
alisema; “Ni kweli huyo mtoto alieleza mambo hayo kwa mjumbe lakini
naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi na mume wangu siyo wachawi, hayo
ni maneno ya uzushi tu, watu wa kijiji hiki wanatuonea wivu kwa sababu
tuna maendeleo kwani hawapendi mtu awe na mafanikio,” alisema.
No comments:
Post a Comment