Wakosoaji wa Mugabe wanasema sera ya mageuzi ya mashamba
ilimalizika miaka miwili iliyopita
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu
waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.
"hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu,
lazima waondoke,'' Mugabe aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.
Chama cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe
yanasikitisha sana na kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.
Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka
kumiliki mashamba yote yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuzorota
kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 200-2009
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90, ametawala Zimbabwe
tangu nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1980.
Alichaguliwa tena mwaka jana kwa asilimia 61 ya kura, na
kumshinda mpinzani wake wa jadi Morgan Tsvangirai.
Chama cha Mugabe pia kilishinda viti vingi vya bunge na
kupata 160 kati ya viti 210.
Mdadisi wa kisiasa nchini humo Stanley Kwenda anasema kuwa
matamshi ya Mugabe, yanashangaza sana kwani serikali ilimaliza mageuzi ya sera
ya umiliki wa mashamba miaka miwili iliyopita.
Inaonekana kwamba Mugabe anataka kuhujumu hali mbaya ua
kiuchumi nchini humo kwa kuzungumzia maswala mengine ambayo hayana umuhimu kwa
sasa.
Wananchi wa Zimbabwe wanakumbwa na kiwango kikubwa cha
ukosefu wa ajira na kufungwa kwa makampuni .
'Wasiwasi'
Mkulima huyu mzungu Zimbabwe,anatizama uharibifu uliofanyiwa
nyumba yake baada ya watu kuivamia
"usiwe mkarimu sana kwa wakulima wazungu. Mashamba ni
yako sio yao,'' alisema Mugabe
alipotembelea mkoa wa Mashonaland , Magharibi
mwa nchi.
Mtamshi ya Rais Mugabe, yalisababisha wasiwasi miongoni mwa
wakulima wazungu. Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa wakulima wazungu
Hendricks Olivier.
Ni wakulima 100 hadi 150 wazungu waliosalia nchini Zimbabwe,
alisema Hendricks.Maelfu ya wakulima walilazimika kuyaacha mashamba yao na
kurejea walikotoka baada ya serikali kufanya mageuzi ya sera ya umiliki wa
ardhi miaka 15 iliyopita.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment