Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati
alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari
alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945,
Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi
kutembea.
Muonekano wa gari hilo kwa ubavuni kulia.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa
Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
ILIKUWAJE?
Habari zilidai kuwa gari hilo halikuwa na matatizo
hivyo
kumfanya dereva wake kukanyaga mafuta kwa
wastani wa kilometa 120 kwa saa.“Sasa
walipofika eneo la Kibaigwa, walikutana na lori likitokea Dodoma kwenda
Morogoro, wakavaana kwa mbele. Nadia likatoka barabarani hadi porini likiwa
limeharibika kuanzia kwenye shoo ya mbele, injini na siti za mbele halafu lori
hilo likakimbia.
“Nadia ilipotulia, Bahati alijikuta hawezi kufanya chochote,
dereva wake naye ameumia kwenye vidole vya miguu. Wale wawili waliokuwa siti ya
nyuma, wote walijeruhiwa lakini mmoja si sana. Ilibidi yeye abaki pale na gari
ili majeruhi wengine wakimbizwe Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, Dodoma kwa
matibabu,” kilisema chanzo hicho.
Gari alilopata nalo ajali mwimbaji wa nyimbo za Injili
Bongo, Bahati Bukuku aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945.
HABARI NYINGINE
Habari ambazo hazijathibitishwa na dereva wa Bahati zilisema kuwa, wakati gari hilo
linakaribiana na lori, dereva wa lori aliwasha taa ‘full’ (mwanga mkali) hivyo
kumfanya dereva huyo kushindwa kuona mbele vizuri, jambo ambalo ni kinyume na
sheria za usalama barabarani.
ROSE MUHANDO, JENNIFER MGENDI WAFUNGA SAFARI
Ilidaiwa kuwa usiku huohuo, waimba Injili mahiri Tanzania,
Rose Muhando na Jennifer Mgendi walipata taarifa za ajali hiyo na kufunga
safari ya kwenda Kongwa kuangalia namna ya kuwahamishia majeruhi hao kwenye
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar.
ROSE MUHANDO
Rose Muhando alipotafutwa kwa simu juzi mchana na kuulizwa
kuhusu kusafiri kwenda Kongwa, alikiri na kusema wameshafika na Jennifer
Mgendi.
“Ndiyo tupo kwenye hekaheka ndugu yangu. Tuna dhamira ya
kuwachukua majeruhi kuwapeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi,” alisema Rose.
JENNIFER MGENDI
Yeye alipopatikana alisema alishtushwa na simu asiyoijua
usiku mnene na kuambiwa shoga yake huyo amepata ajali mbaya ya gari.“Kitu cha
kwanza niliuliza hali yake, nikaambiwa ameumia mgongo, dereva wake mguu. Ndiyo
nikaanza kuwataarifu wadau wengine na mimi kujiandaa kwa safari kutoka Dar kuja
Kongwa usiku huohuo. Kwa kweli ameumia,” alisema Mgendi ambaye ni rafiki mkubwa
wa Bahati.
Naye Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stella Joel
alipozungumza na gazeti hili juzi, alikiri waimba injili hao kuondoka Dar es
Salaam kuelekea Dodoma kumpa msaada mwenzao.
BAHATI BUKUKU AZUNGUMZA KWA TABU
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari hizi alimpigia simu
Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata
tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia
mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa
mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar
tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema
Bahati.
Mwandishi: “Unadhani nani alikuwa na kosa kati ya dereva
wako na wa lori?”Bahati: “Sijui
chochote. Halafu najisikia vibaya sana, tuwasiliane baadaye kaka ‘angu.”
UZOEFU WA DEREVA
Habari zinasema kwamba, Eddy ni dereva wa miaka mingi. Mbali
na jijini Dar, pia amekuwa akiendesha magari kwenda nje ya Tanzania kama
Burundi na Rwanda na katika ajali hiyo alikuwa akienda nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo ana uzoefu wa safari za usiku.
WATU WA INJILI NA AJALI ZA DODOMA
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya kwanza kuripotiwa
kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,
Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana na mwendesha
bodaboda.Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho, kilomita chache kabla ya
kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari lake aina ya Toyota Mark II GX
100.
Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha bodaboda huyo waliumia
sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa
matibabu.
Kabla ajali ya Msama haijapoa, Mei, mwaka huu, Edson
Mwasabwite naye alipata ajali kwenye Barabara Kuu ya Dodoma–Morogoro. Alikuwa akitoka Dodoma
kurudi Dar. Alinusurika.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment