Mwanamke raia wa Sudan aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya
kubadili dini amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa
Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake waliondoka na
ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo
Pistelli.Baada ya kuwasili Italia bi Merian alikutana na Papa Francis ambaye
alimsifu kwa kusimamia dini ya ukristu licha ya tishio la mauti.
Merian alikutana na papa katika makao yake rasmi ya Santa
Marta iliyoko kwenye makao makuu ya kanisa Katoloki ya Vatican.
Mkutano huo ulidumu kwa takriban nusu saa .
Baba wa Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini
hiyo nchini Sudan Meriam pia
ni muislamu na hawezi kubadili dini.Meriam
mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa
muislamu.
Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka
picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea
kutua mjini Roma.Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani
kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda
mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha ghadhabu dunia nzima.Aliachwa
huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.
No comments:
Post a Comment