Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya
hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat,
amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea
majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi
wa Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na
kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango
waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini.
Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha
kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.
Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu
Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki
kigumu.
IMETOLEWA NA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014
No comments:
Post a Comment