BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
Plot No. 8, Block No. 46, Sam Nujoma Road, Mwenge; P.O. Box
76068, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: (General) +255 22 2772432/2772433; Fax: +255 22
2700286; E-mail: info@heslb.go.tz
Website: www.heslb.go.tz
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda
kuwatahadharisha waombaji wa mikopo na umma kwa ujumla, juu ya kuibuka kwa
genge la matapeli wanaowalaghai wananchi ambapo hujitambulisha kuwa wao ni
wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo.
Mbinu zinazotumiwa na genge hilo la matapeli ni kuwatumia
ujumbe mfupi wa simu waombaji wa mikopo ukiwatahadharisha kuwa fomu zao za
maombi ya mikopo zina dosari na hivyo wanatakiwa watume sh. 15,000.00 kwa
kutumia utaratibu wa kutuma Fedha kwa njia ya mitandao ya simu kwenda kwenye
namba za simu za matapeli hao ili fomu zao za mikopo ziweze kufikiriwa.
Katika utapeli huo,
matapeli hao wanawatishia waombaji wa Mikopo wanaoendelea na masomo kuwa
wasipohuisha taarifa zao za kuendelea kupokea Mikopo mwaka ujao wa kitaaluma
2014/2015 hawatapata Mikopo.
Bodi ya Mikopo
inapenda kuwafahamisha waombaji wa Mikopo na umma kwa ujumla kwamba:
(i) Waombaji
mikopo wanatakiwa kutuma fomu zao au taarifa zilizokosekana kwa njia ya Posta
tu. Bodi haijaweka wakala mwingine yeyote anayetoza ada kwa ajili hiyo.
(ii) Ada zote
za maombi ya mikopo zilielekezwa kulipwa kwa njia ya M-Pesa kwa utaratibu ambao
umeelekezwa bayana kwenye ukurasa wa maombi kwa njia ya mtandao
(http://olas.heslb.go.tz) na si vinginevyo.
(iii) Waombaji
wa Mikopo wanaoendelea na masomo hawatakiwi kujaza fomu za maombi ya Mikopo
kama ilivyokwisha kufafanuliwa katika Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa mwaka wa
masomo 2014/2015.
(iv) Waombaji
mikopo watakaopokea simu au ujumbe mfupi wa simu unaowataka watume Fedha ili
wapatiwe huduma ya kuhuisha taarifa zao za mkopo watoe taarifa kuhusu matapeli
hao kwa Polisi au TAKUKURU kusudi hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya
wahalifu hao.
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment