Kufuatia
tatizo kubwa la maji linaloikabili nchi ya India, wanasayansi wameweza
kuitumia vizuri teknolojia na kuanzisha ATM zinazotoa maji kama ATM
zinazotoa pesa tulizozizoa. Kufuatia
teknolojia hiyo, mwananchi wa kawaida anajiandisha na kupewa ATM kadi
maalum ambayo atakuwa anaitumia kupata lita za maji anazotaka kulingana
na kiwango cha pesa anacholipa. Mteja anaweza kupata huduma hii masaa
24.
Mteja pia ana nafasi nyingine ya kutumia sarafu kwa kuingiza kwenye ATM hiyo na kuweka kiwango cha lita za maji anazotaka. ATM hizo zinatoa maji safi na salama kwa matumizi ya kunywa kwa kuwa zimefungiwa mtambo maalum wa kusafisha na kuchuja maji.
Mradi huo ulianzishwa mwaka 2010 na kampuni ya ‘Sarvajal’ ambayo jina lake lina maana ya ‘maji kwa wote’, na umelenga zaidi kuwapa nafuu wananchi wa kawaida hasa waishio vijijini. Na mwaka 2010 ulitoa huduma kwa zaidi ya wananchi 70,000.
Hadi sasa mradi huo umekuwa mkubwa na unahudumia watu wengi zaidi na makampuni mengi yamewekeza. Inaelezwa kuwa kuna makampuni ambayo yanatumia teknolojia hiyo pia kusambaza maziwa (ATM ya Maziwa).
Mtanzania hapo vipi….!?
No comments:
Post a Comment