Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017
waliangamia jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi
ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi
hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao
wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo
iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon ,
Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve
alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso
, Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga.
No comments:
Post a Comment