Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana
kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha
tohara wavulana.
Tohara hiyo ni utamaduni unaopewa heshima kubwa katika
baadhi ya maeneo ya taifa hilo.
Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni
njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni
huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za
siri kuoza na majerahe mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara
ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama
hivyo.
Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka
na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya
idhini ya wazazi.Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye
uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.Mwezi
jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za
kupashwa tohara.
No comments:
Post a Comment