Wachezaji saba wa Ujerumani, wanaugua mafua , saa 24 kabla
ya mechi yao ya robo fainali dhidi ya Ufaransa.
Kocha Joachim Low anasema kuwa wengi wanaumwa na koo ingawa
hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa.
"Ni mapema sana kufanya uamuzi wowote kuhusu orodha ya
wachezaji watakaoingia uwanjani, '' alisema Low
Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii
huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria Jumatatu.
Low anaamini kuwa mazingira ya Brazil na safari za hapa na
pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu ya wachezaji wake kuugua.
Lakini aliongeza kuwa , hali sio mbaya sana , sitaki watu
wadhani kuwa tunakabiliwa na wakati mgumu, hapana, '' alinukuliwa akisema Low
Chanzo:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment