Pages

Wednesday, July 2, 2014

WAZIRI CHIKAWE, IGP MANGU WAFANYA ZIARA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA KUANGALIA USALAMA

 Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakizunguka katika viwanja vya Sabasaba katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka kwenye Banda la Wizara yake wakati wa  Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka na kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo kuangalia hali ya usalama. 

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquline Maleko akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe  (wapili kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto) na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) jinsi Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walivyojipanga kuimarisha usalama katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa

No comments:

Post a Comment