Pages

Thursday, August 21, 2014

AFYA LEO::ZIJUE RANGI ZA HAJA NDOGO (MKOJO) NA MAANA YAKE KI-AFYA



1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):

Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo


2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo: 
Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.



3. Manjano iliyo pauka:

Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha



4. Njano iliyo kolea:

Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.


5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali:

Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.


6. Rangi ya Kahawia:

Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kama hali hii ikiendelea.



7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu:

Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya wekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.


No comments:

Post a Comment