Mchina aliyekuwamo kwenye gari akizungumza kwa simu, pembeni yake ni askari wa usalama barabarani.
Watu
watatu akiwemo raia wa China na dereva ambaye ni mtanzania wamenusurika
kufa katika ajali iliyotokea maeneo ya Millennium Tower, Kijitonyama
jijini Dar es Salaam ikihusisha gari ndogo aina ya Opa.
Dereva wa Opa ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la zimamoto
lililokuwa linatokea njia ya Mikocheni kuingia barabara kubwa.
“Gari
la fire lilikuwa kasi sana huku likipiga king’ora, kwa hiyo kujihami
dereva mwenye Opa akajikuta ameingia mtaroni, tunashukuru hakuna
aliyeumia,’’ alisema Robert.
Aidha
mtu mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo ni Abdukarim ambaye
alikuwa ndani ya mtaro huo akisafisha. Askari wa usalama barabarani
alifika eneo la tukio huku break down likianza kuitoa gari hiyo mtaroni.
Gari la break down likivuta Opa iliyoingia mtaroni.
Aliyenusurika katika ajali hiyo, Abdukarim akiwa pembeni akitafakali.
No comments:
Post a Comment