Pages

Saturday, August 23, 2014

ATLETICO MADRID WAICHAPA REAL MADRID 1-0, YABEBA SUPER CUP HISPANIA

Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid.
Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou.Atletico Madrid
Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu.
Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo.
Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.





No comments:

Post a Comment