Kiungo mshambuliaji mpya wa Manchester United, Angel Di Maria ameandika barua iliyowasikitisha wachezaji na mashabiki wa Real Madrid.
Di Maria ambaye ametua Man United kwa dau la pauni milioni 60 ambalo ni rekodi England, amesema hakupanga kuiacha timu hiyo ya Hispania.
Mashabiki waliochangia kwenye mtandao wa Twitter wameelezwa kusikitishwa na barua hiyo huku wakiamini siku moja, Di Maria atarejea tena katika klabu yao.
Amesema wakati anakwenda kwenye Kombe la dunia baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya ‘La Decima’ akiwa na Madrid, alitarajia kurudi na kuendelea na kazi yake.
“Hata hivyo kuna mambo yalijitokeza, yakiwemo ya mshahara wangu na sasa natarajia kuyapata Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani na nina imani nitaweka historia pale,” alieleza katika sehemu ya barua hiyo.
Di Maria ameeleza atakavyowakumbuka wachezaji wengi wa Madrid na maisha yao kwa ujumla.
Tayari Muargentina huyo amemalizana na Man United na baadhi ya wachezaji wa Madrid kama Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, hawakutaka aondoke.
No comments:
Post a Comment