Pages

Friday, August 29, 2014

Brad Pitt na Angelina Jolie waoana


Jolie na Pit walichumbiana mwaka 2012
Brad Pitt na Angelina Jolie wameoana rasmi , kulingana na msemaji wao.
Pitt, mwenye umri wa miaka 50 na Jolie mwenye umri wa miaka 39, walifunga pingu za maisha nchini Ufaransa Jumamosi na kumaliza miaka mingi ya suitofahamu ikiwa watawahi kuoana.

 
Waigizaji hao inaarifiwa walioana katika sherehe iliyofanywa kimya kimya katika kanisa ndogo eneo la Chateau Miraval Ufaransa.
Sherehe hio ilifanyika kwa faragha na kuhudhuriwa tu na familia za wawili hao pamoja na marafiki zao.
Watoto wao pia walihusishwa katika sherehe hiyo.
Jolie aliambatana na wanawe wakubwa wa kiume, Maddox na Pax, wenye umri wa miaka 13 na 10 mtawalia.
Watoto wao wa kike Zahara na Vivienne, wote waliwarushia mauwa wazazi wao walipokuwa wanatembea kuelekea kanisani. Inaarifiwa sherehe hiyo haikufuata dini yoyote.
Wacheza filamu hao walianza uhusiano wao wa kimapenzi mwaka 2005 walipoigiza katika filamu ya 'Mr and Mrs Smith'. Walichumbiana Aprili mwaka 2012.

Kabla ya ndoa yake kwa Jolie, Pit alikuwa amemuoa muigizaji, Jennifer Aniston, wakati Jolie alikuwa ameolewa na Jonny Lee Miller na Billy Bob Thornton. Ndoa yake kwa wawili hao ilivunjika.

No comments:

Post a Comment