Jeshi la polisi Mkoani Iringa linamtafuta dereva wa pikipiki kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu kwa ajali ya barabarani kisha kukimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Mfaume Kilangi ambaye pia ni mwenyekitio wa kijiji cha Idodi wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa akiwa anaendesha pikipiki ambayo haijafahamika namba zake za usajili ilimgonga na kusababisha kifo cha Laurent Kafwela umri miaka 40.
Aidha ameongeza kuwa marehemu amefariki muda mfupi akiwa anakimbizwa katika hospitari ya Mapogoro wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa wa Iringa na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa kutochukua tahadhari kwenye makazi ya watu.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema ajari hiyo imetokea katika eneo la Mapogoro katika barabara ya Idodi-Tagamenda wilaya ya Iringa Vijijini pia ametoa wito kwa wamiliki na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajari zinazoweza kuepukika
No comments:
Post a Comment