Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 11, 2014

HAWA NDIO WACHEZAJI AMBAO KOCHA WA MANCHESTER UNITED KAWAAMBIA MILANGO IKO WAZI WAONDOKE

You can stay: United boss Louis van Gaal has informed Kagawa he has a future role at Old TraffordRafael da Silva, Marouane Fellaini, Luis Nani, Oliviera Anderson, Wilfried Zaha,Will Keane na Javier Hernandez wameambiwa na Meneja wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal kuwa wanaweza kuondoka klabuni hapo kwakuwa hawako ndani ya mipango ijayo ya Manchester United.

Heading for the exit: Javier Hernandez has been told he can leave Manchester United 
Van Gaal jana amekutana na mchezaji mmoja mmoja binafsi kwa malengo ya kuzungumza 

 
nao na amewaarifu wachezaji Fellaini, Zaha, Nani na Keane kwamba klabu itakuwa tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu yoyote ile itakayokuwa inawahitaji.


Nani of Manchester United featured against Inter Milan in pre-season

Rafael, ni moja kati ya majina ambayo yamewaacha midomo wazi wadadisi wengi wa masuala ya soka kwani hakuna aliyetarajia kuwa angeweza kuoneshwa mlango wa kutokea na Van Gaal.Inasemekana kuwa LvG anataka kumtafuta mlinzi wa pembeni mwingine ambaye ndiye atakua mbadala wa Rafael.

 Rafael played for United in pre-season against LA Galaxy

 Kagawa mmoja kati ya wachezaji ambao walikua wakitajwa sana kuwa wataoneshwa mlango wa kutokea ndani ya United amenusurika kwenye kadhia hiyo kwani sasa atakua msaidizi wa Wahispania  Ander Herrera na Juan Mata kwenye sehemu ya kiungo cha ushambulizi.

 Marouane Fellaini will be sold just a year after joining United for £27million

 Kiungo Olivieira Anderson na mshambuliaji  Javier Hernandez wote walikua wakifahamu kuwa United ilikuwa iko tayari kusikiliza ofa kutoka kwa vilabu vya  Southampton, Inter Milan, Tottenham, Atletico Madrid na Juventus ambavyo vilionesha kumuhitaji Chicharito wakati  Napoli inamuhitaji  Fellaini ambaye inasemekana kuwa United ndio wanaouchelewesha mchongo huo kukamilika.

Newcastle imeonesha kumuhitaji sana Wilfred Zaha, sambamba na vilabu vya Crystal Palace, West Ham na Nottingham Forest.

No comments:

Post a Comment